Judges 7:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gideoni akatuma wajumbe kote katika nchi ya milima ya Efraimu watangaze: “Teremkeni kuwakabili Wamidiani na kuwazuia kwa kuteka vijito na mto Yordani mpaka Beth-bara.” Basi, wanaume wote wa Efraimu wakaja na kuuteka mto Yordani mpaka Beth-bara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima ya Efraimu, akisema, “Teremkeni dhidi ya Wamidiani na mkazuie vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.” Hivyo wanaume wote wa Efraimu wakakutanika pamoja na kuzingira vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Gideoni akapeleka wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, telemkeni juu ya Midiani, na kuyashika hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani. Basi watu waume wote wa Efraimu walikutana pamoja, wakayashika maji mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gideoni akatuma wajumbe kote katika nchi ya milima ya Efraimu watangaze: “Teremkeni kuwakabili Wamidiani na kuwazuia kwa kuteka vijito na mto Yordani mpaka Beth-bara.” Basi, wanaume wote wa Efraimu wakaja na kuuteka mto Yordani mpaka Beth-bara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vya Efraimu akisema, “Telemkeni dhidi ya Wamidiani na mkazuie vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.” Hivyo watu wote wa Efraimu wakakutanika pamoja na kuzingira mto wa Yordani hadi Beth-Bara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vya Efraimu akisema, “Teremkeni dhidi ya Wamidiani na mkazuie vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.” Hivyo watu wote wa Efraimu wakakutanika pamoja na kuzingira mto wa Yordani hadi Beth-Bara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, teremkeni juu ya Midiani, na kuyatwaa hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana huo mto wa Yordani. Basi wanaume wote wa Efraimu walitokeza wakayatwaa maji mpaka Bethbara, yaani, huo mto wa Yordani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gideoni akatuma wajumbe kote katika nchi ya milima ya Efraimu watangaze: “Teremkeni kuwakabili Wamidiani na kuwazuia kwa kuteka vijito na mto Yordani mpaka Beth-bara.” Basi, wanaume wote wa Efraimu wakaja na kuuteka mto Yordani mpaka Beth-bara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Gideoni akatuma wajumbe kwenda milimani po pote kwa Efuraimu kwamba: Shukeni kuwajia Wamidiani, mfike mbele yao kwenye maji ya Beti-Bara, hata kwenye Yordani. Watu wote wa Efuraimu wakaitikia, wakapapata pote palipo penye maji mpaka Beti-Bara, nao Yordani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Gideoni akapeleka wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, telemkeni juu ya Midiani, na kuyashika hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani. Basi watu waume wote wa Efraimu walikutana pamoja, wakayashika maji mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gideoni akatuma wajumbe katika inchi yote ya milima ya Efuraimu watangaze: “Muteremuke kwa kuwafuata Wamidiani na kuwazuia kwa kuteka vijito na muto Yordani mpaka Beti-Bara.” Basi, wanaume wote wa Efuraimu wakakuja na kuuteka muto Yordani mpaka Beti-Bara.