Judges 7:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakachukua mateka viongozi wawili wa Midiani, yaani Orebu na Zeebu. Wakamuua Orebu katika mwamba wa Orebu, naye Zeebu wakamuua katika shinikizo la Zeebu, wakiwa wanawafuatia Wamidiani. Wakamletea Gideoni vichwa vya Orebu na Zeebu, ngambo ya mto Yordani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakawakamata Orebu na Zeebu, wakuu wawili wa Midiani. Wakamuua Orebu pale penye mwamba wa Orebu, na Zeebu wakamuua pale penye shinikizo la kukamulia zabibu la Zeebu. Wakawafuatia Wamidiani na kuleta vichwa vya Orebu na Zeebu kwa Gideoni, huko ng’ambo ya Yordani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng'ambo ya pili ya Yordani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakachukua mateka viongozi wawili wa Midiani, yaani Orebu na Zeebu. Wakamuua Orebu katika mwamba wa Orebu, naye Zeebu wakamuua katika shinikizo la Zeebu, wakiwa wanawafuatia Wamidiani. Wakamletea Gideoni vichwa vya Orebu na Zeebu, ng'ambo ya mto Yordani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakawakamata wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamwulia Orebu pale penye mwamba wa Orebu, na Zeebu wakamwulia penye shinikizo la kukamulia divai la Zeebu. Wakawafuatia Wamidiani na kuleta vichwa vya Orebu na Zeebu kwa Gideoni, huko ng'ambo ya Yordani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakawakamata wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamuulia Orebu pale penye mwamba wa Orebu, na Zeebu wakamuulia penye shinikizo la kukamulia divai la Zeebu. Wakawafuatia Wamidiani na kuleta vichwa vya Orebu na Zeebu kwa Gideoni, huko ng’ambo ya Yordani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng'ambo ya pili ya Yordani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakachukua mateka viongozi wawili wa Midiani, yaani Orebu na Zeebu. Wakamuua Orebu katika mwamba wa Orebu, naye Zeebu wakamuua katika shinikizo la Zeebu, wakiwa wanawafuatia Wamidiani. Wakamletea Gideoni vichwa vya Orebu na Zeebu, ngambo ya mto Yordani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakamata wakuu wawili wa Midiani, Orebu (Kunguru) na Zebu (Chui), wakamwua Orebu penye Mwamba wa Kunguru, naye Zebu wakamwua penye Kamulio la Chui. Walipokwisha kuwafukuza Wamidiani, wakavichukua vichwa vyao Orebu na Zebu ng'ambo ya huko ya Yordani, wakampelekea Gideoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng’ambo ya pili ya Yordani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakatwaa mateka viongozi wawili wa Midiani, majina yao ni Kibombobombo na Imbwa-wa-Pori. Wakamwua Kibombobombo juu ya jiwe la Kibombobombo, naye Imbwa-wa-Pori wakamwua katika kikamulio cha Imbwa-wa-Pori wakiwa wanawafuatilia Wamidiani. Wakamuletea Gideoni vichwa vya Kibombobombo na Imbwa-wa-Pori, ngambo ya muto Yordani.