Judges 7:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Gideoni akawapeleka watu mtoni na Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Watu watakaoramba maji kama mbwa, utawatenganisha na wale watakaopiga magoti kunywa maji.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gideoni akalipeleka lile jeshi kwenye maji, naye Mwenyezi Mungu akamwambia Gideoni, “Watenganishe watakaoramba maji kwa ulimi kama mbwa, na wale watakaopiga magoti ili kunywa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akawaleta watu chini majini. Bwana akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Gideoni akawapeleka watu mtoni na Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Watu watakaoramba maji kama mbwa, utawatenganisha na wale watakaopiga magoti kunywa maji.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Gideoni akalileta lile jeshi chini kwenye maji naye BWANA akamwambia Gideoni, “Watenge upande mmoja wale wote wanywao maji kwa ulimi, kama vile mbwa anywavyo, wale wote wapigao magoti ili kunywa wakipeleka mikono yao vinywani mwao, waweke upande mwingine.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Gideoni akalileta lile jeshi chini kwenye maji naye bwana akamwambia Gideoni, “Watenge upande mmoja wale wote wanywao maji kwa ulimi, kama vile mbwa anywavyo, wale wote wapigao magoti ili kunywa wakipeleka mikono yao vinywani mwao, waweke upande mwingine.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akawaleta watu chini majini. BWANA akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Gideoni akawapeleka watu mtoni na Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Watu watakaoramba maji kama mbwa, utawatenganisha na wale watakaopiga magoti kunywa maji.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowatelemsha watu kufika penye maji, naye Bwana akamwambia Gideoni: Kila atakayelamba maji kwa ulimi wake, kama mbwa anavyolamba, umweke mahali pake! Vilevile kila atakayepiga magoti yake, apate kunywa, umweke pake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akawaleta watu chini majini. BWANA akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Gideoni akawapeleka watu kwenye muto na Yawe akamwambia: “Watu watakaolamba maji kwa ulimi kama imbwa, utawatenganisha na wale watakaopiga magoti kwa kunywa maji.”