Judges 7:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Idadi ya waliokunywa maji kwa kuchota kwa mikono yao na kuramba kama mbwa ilikuwa 300. Lakini wengine wote waliobaki walipiga magoti kunywa maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliokunywa kwa kuramba maji kutoka mikononi mwao walikuwa watu mia tatu. Wengine wote walipiga magoti ili kunywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Idadi ya waliokunywa maji kwa kuchota kwa mikono yao na kuramba kama mbwa ilikuwa 300. Lakini wengine wote waliobaki walipiga magoti kunywa maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Idadi ya wale waliokunywa kwa kulamba lamba walikuwa 300, lakini wengine wote katika jeshi walipiga magoti ili kunywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Idadi ya wale waliokunywa kwa kuramba ramba walikuwa 300, lakini wengine wote katika jeshi walipiga magoti ili kunywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Idadi ya waliokunywa maji kwa kuchota kwa mikono yao na kuramba kama mbwa ilikuwa 300. Lakini wengine wote waliobaki walipiga magoti kunywa maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, hesabu yao waliolamba maji wakiyapleeka vinywani kwa viganja ikawa watu 300; wengine wote walipiga magoti yao, wapate kunywa maji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jumla ya waliokunywa maji kwa kuchota kwa mikono yao na kulamba kama imbwa ilikuwa mia tatu. Lakini wengine wote waliobaki walipiga magoti kwa kunywa maji.