Judges 8:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gideoni akarudi kwa watu wa Sukothi, akawaambia, “Si mtakumbuka mlivyonitukana mliposema, ‘Kwa nini tuwape mikate watu wako waliochoka sana nanyi bado hamjamshinda Zeba na Salmuna?’ Haya basi, Zeba na Salmuna ndio hawa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia wanaume wa Sukothi, “Tazameni Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, tayari umewakamata Zeba na Salmuna ili tulipatie jeshi lako mikate?’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akawafikilia wale watu wa Sukothi, akawaambia, Tazama, Zeba na Salmuna, ambao ninyi mlinisimanga kwa ajili yao, mliposema, Je! Mikono ya Zeba na Salmuna iko sasa mikononi mwako wewe, hata tuwape watu wako waliochoka mikate?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gideoni akarudi kwa watu wa Sukothi, akawaambia, “Si mtakumbuka mlivyonitukana mliposema, ‘Kwa nini tuwape mikate watu wako waliochoka sana nanyi bado hamjamshinda Zeba na Salmuna?’ Haya basi, Zeba na Salmuna ndio hawa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia watu wa Sukothi, “Tazama, hapa wapo Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia watu wa Sukothi, “Tazama, hapa wapo Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akawafikia wale watu wa Sukothi, akawaambia, Tazama, Zeba na Salmuna, ambao ninyi mlinisimanga kwa ajili yao, mliposema, Je! Mikono ya Zeba na Salmuna iko sasa mikononi mwako wewe, hata tuwape watu wako waliochoka mikate?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gideoni akarudi kwa watu wa Sukothi, akawaambia, “Si mtakumbuka mlivyonitukana mliposema, ‘Kwa nini tuwape mikate watu wako waliochoka sana nanyi bado hamjamshinda Zeba na Salmuna?’ Haya basi, Zeba na Salmuna ndio hawa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika kwao wale watu wa Sukoti akawaambia: Watazameni akina Zeba na Salmuna, ambao mlinisimanga kwa ajili yao kwamba: Je? Makonde ya Zeba na ya Salmuna yamo sasa mkononi mwako, tuwape mikate watu wako waliochoka?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akawafikilia wale watu wa Sukothi, akawaambia, Tazama, Zeba na Salmuna, ambao ninyi mlinisimanga kwa ajili yao, mliposema, Je! Mikono ya Zeba na Salmuna iko sasa mikononi mwako wewe, hata tuwape watu wako waliochoka mikate?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gideoni akarudi kwa watu wa Sukoti, akawaambia: “Si mutakumbuka mulivyonitukana muliposema: ‘Kwa nini tuwape mikate watu wako waliochoka sana nanyi hamujamushinda Sadaka na Kivuli?’ Haya basi, Sadaka na Kivuli ndio hawa.”