Judges 8:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akawachukua wazee wa Sukothi na kuwapa funzo wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na mbigili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawachukua hao wazee wa mji, na kuwaadhibu wanaume wa Sukothi kwa kuwachapa kwa miiba na michongoma ya nyikani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akawatwaa hao wazee wa mji, na miiba ya nyikani na michongoma, akawafunza hao watu wa Sukothi kwayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akawachukua wazee wa Sukothi na kuwapa funzo wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na mbigili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawachukua hao viongozi wa mji na kuwafundisha watu wa Sukothi somo kwa kuwaadhibu kwa miiba na michongoma ya nyikani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawachukua hao viongozi wa mji na kuwafundisha watu wa Sukothi somo kwa kuwaadhibu kwa miiba na michongoma ya nyikani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akawatwaa hao wazee wa mji, na miiba ya nyikani na michongoma, akawafunza hao watu wa Sukothi kwayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akawachukua wazee wa Sukothi na kuwapa funzo wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na mbigili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawachukua wazee wa mji na miiba ya nyikani na mikunju, akaitumia ya kuwafundisha watu wa Sukoti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akawatwaa hao wazee wa mji, na miiba ya nyikani na michongoma, akawafunza hao watu wa Sukothi kwayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akawatwaa wazee wa Sukoti na kuwapa fundisho wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na michongoma.