Judges 8:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uzito wa vipuli vyote alivyowataka wampe ulikuwa kilo ishirini. Zaidi ya hivyo, alipokea pia herini, mavazi ya urujuani yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani na mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uzito wa pete za dhahabu alizoomba ulikuwa shekeli elfu moja na mia saba, bila kuhesabu mapambo mengine, vidani, na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na uzani wa hizo pete za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uzito wa vipuli vyote alivyowataka wampe ulikuwa kilo ishirini. Zaidi ya hivyo, alipokea pia herini, mavazi ya urujuani yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani na mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilifikia shekeli 1,700, bila kuhesabu mapambo mengine, pete za masikio na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilifikia shekeli 1,700, bila kuhesabu mapambo mengine, pete za masikio na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na uzani wa hizo herini za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uzito wa vipuli vyote alivyowataka wampe ulikuwa kilo ishirini. Zaidi ya hivyo, alipokea pia herini, mavazi ya urujuani yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani na mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uzito wa haya mapete ya dhahabu ya masikioni, aliyoyataka, ukawa mzigo mkubwa wa mtu (sekeli 1700 za dhahabu, ndio ratli 62) pasipo manyamwezi na mapambo mengine ya masikioni na mavazi ya kifalme, wafalme wa Wamidiani waliyoyavaa, tena pasipo mikufu ya shingoni pa ngamia wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na uzani wa hizo pete za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uzito wa pete zote alizoomba wamupe ulikuwa kilo makumi mbili. Zaidi ya hivyo, alipokea vilevile vyuma vya masikio, nguo za rangi nyekundu-nyeusi zilizovaliwa na wafalme wa Midiani na mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia wao.