Judges 9:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mti wa miiba ukajibu, ‘Kama kweli mnataka kuniteua kuwa mfalme, njoni mkae chini ya kivuli changu. Lakini kama hamtaki kufanya hivyo, basi moto na utoke kwenye miiba yangu na kuiteketeza hata mierezi ya Lebanoni.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nao mchongoma ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka kunitawaza niwe mfalme wenu, basi njooni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mchongoma ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mti wa miiba ukajibu, ‘Kama kweli mnataka kuniteua kuwa mfalme, njoni mkae chini ya kivuli changu. Lakini kama hamtaki kufanya hivyo, basi moto na utoke kwenye miiba yangu na kuiteketeza hata mierezi ya Lebanoni.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nao mti wa miiba ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka niwe mfalme wenu, basi njoni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mti wa miiba ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nao mti wa miiba ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka niwe mfalme wenu, basi njooni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mti wa miiba ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Ikiwa kwa kweli mnanitia mafuta niwe mfalme juu yenu, basi njoni mkakae chini ya kivuli changu; la sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mti wa miiba ukajibu, ‘Kama kweli mnataka kuniteua kuwa mfalme, njoni mkae chini ya kivuli changu. Lakini kama hamtaki kufanya hivyo, basi moto na utoke kwenye miiba yangu na kuiteketeza hata mierezi ya Lebanoni.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mchongoma ukaiambia miti: Kama mnataka kweli kunipaka mafuta, niwe mfalme wenu, njoni, mkae pasipo woga kivulini pangu! Kama hamtaki, moto na utoke katika mchongoma, uile miangati ya Libanoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muti wa miiba ukajibu: ‘Kama kweli munataka kunichagua kuwa mufalme, mukuje mukae chini ya kivuli changu. Lakini kama hamutaki kufanya hivyo, basi moto utoke kwenye miiba yangu na kuiteketeza hata mierezi ya Lebanoni.’ ”