Judges 9:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yothamu akaendelea kusema, “Sasa basi, mnadhani mmefanya Abimeleki mfalme kwa nia njema na uaminifu? Je, mnadhani mmemtendea wema Yerubaali na jamaa yake kama alivyostahili kwa matendo yake?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi, je, mmetenda kwa uaminifu na heshima kwa kumtawaza Abimeleki kuwa mfalme? Je, mmetendea mema Yerub-Baali na jamaa yake, na mkamtendea kama alivyostahili?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa ikiwa mmetenda kwa uaminifu na uelekevu, katika kumtawaza Abimeleki awe mfalme, na ikiwa mmemtendea mema Yerubaali na nyumba yake, na kumtendea kama ilivyostahili mikono yake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yothamu akaendelea kusema, “Sasa basi, mnadhani mmefanya Abimeleki mfalme kwa nia njema na uaminifu? Je, mnadhani mmemtendea wema Yerubaali na jamaa yake kama alivyostahili kwa matendo yake?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Basi ikiwa mmetenda kwa uaminifu na heshima kumfanya Abimeleki kuwa mfalme, na kama mmetendea vyema Yerub-Baali na jamaa yake kama ilivyostahili:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi ikiwa mmetenda kwa uaminifu na heshima kumfanya Abimeleki kuwa mfalme, na kama mmetendea vyema Yerub-Baali na jamaa yake kama ilivyostahili:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa ikiwa mmetenda kwa nia njema na uzingativu, katika kumtawaza Abimeleki awe mfalme, na ikiwa mmemtendea mema Yerubaali na nyumba yake, na kumtendea kama ilivyostahili mikono yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yothamu akaendelea kusema, “Sasa basi, mnadhani mmefanya Abimeleki mfalme kwa nia njema na uaminifu? Je, mnadhani mmemtendea wema Yerubaali na jamaa yake kama alivyostahili kwa matendo yake?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa ninyi je? Mmejitokeza kuwa wenye kweli na welekevu mlipomfanya Abimeleki kuwa mfalme? Au Yerubaali nao walio wa mlango wake mmewatendea mema na kuwafanyizia, kama mikono yake ilivyowafanyizia ninyi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa ikiwa mmetenda kwa uaminifu na uelekevu, katika kumtawaza Abimeleki awe mfalme, na ikiwa mmemtendea mema Yerubaali na nyumba yake, na kumtendea kama ilivyostahili mikono yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yotamu akaendelea kusema: “Sasa basi, munazani mumefanya Abimeleki mufalme kwa nia njema na uaminifu? Munazani mumemutendea wema Yerubali na jamaa yake kama alivyostahili kwa matendo yake?