Judges 9:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini leo mmeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana sabini juu ya jiwe moja, halafu mmemfanya Abimeleki mtoto wa mjakazi wa baba, awe mfalme wa wakazi wa Shekemu kwa sababu tu ni mtu wa ukoo wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja. Nanyi mmemtawaza Abimeleki mwana wa mjakazi wake kuwa mfalme juu ya wenyeji wa Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa sababu yeye ni ndugu yenu;)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini leo mmeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana sabini juu ya jiwe moja, halafu mmemfanya Abimeleki mtoto wa mjakazi wa baba, awe mfalme wa wakazi wa Shekemu kwa sababu tu ni mtu wa ukoo wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja, nanyi mkamfanya Abimeleki mwana wa mwanamke mtumwa kuwa mfalme juu ya Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja, nanyi mkamfanya Abimeleki mwana wa mwanamke mtumwa kuwa mfalme juu ya Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa sababu yeye ni ndugu yenu;)
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini leo mmeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana sabini juu ya jiwe moja, halafu mmemfanya Abimeleki mtoto wa mjakazi wa baba, awe mfalme wa wakazi wa Shekemu kwa sababu tu ni mtu wa ukoo wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi mmeuinukia leo mlango wa baba yangu mkiwaua wanawe 70 juu ya jiwe moja, mkamfanya Abimeleki, mwana wa kijakazi wake, kuwa mfalme wa wenyeji wa Sikemu, kwa kuwa ni ndugu yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa sababu yeye ni ndugu yenu;)
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini leo mumeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana makumi saba juu ya jiwe moja, halafu mumemufanya Abimeleki mutoto wa mujakazi wa baba, akuwe mufalme wa wakaaji wa Sekemu kwa sababu tu ni mutu wa ukoo wenu.