Judges 9:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Semeni papa hapa mbele ya wananchi wote wa Shekemu: Lipi ni jema kwenu, kwamba watoto wote sabini wa kiume wa Yerubaali wawatawale au mtoto mmoja? Kumbukeni kuwa mimi ni damu yenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waulizeni watu wote wa Shekemu, ‘Lipi lililo bora kwenu: Kutawaliwa na wana wote sabini wa Yerub-Baali, au mtu mmoja peke yake?’ Kumbukeni kwamba mimi ni mwili wenu na damu yenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya, neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Semeni papa hapa mbele ya wananchi wote wa Shekemu: Lipi ni jema kwenu, kwamba watoto wote sabini wa kiume wa Yerubaali wawatawale au mtoto mmoja? Kumbukeni kuwa mimi ni damu yenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Waulizeni watu wote wa Shekemu, ‘Lipi lililo bora kwenu: Kutawaliwa na wana wote sabini wa Yerub-Baali, au mtu mmoja peke yake?’ Kumbukeni kwamba, mimi ni mfupa wenu nyama yenu hasa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waulizeni watu wote wa Shekemu, ‘Lipi lililo bora kwenu: Kutawaliwa na wana wote sabini wa Yerub-Baali, au mtu mmoja peke yake?’ Kumbukeni kwamba, mimi ni mfupa wenu nyama yenu hasa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya, neneni tafadhali masikioni mwa wanaume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo bora kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, wawatawale, au kwamba mtu mmoja awatawale? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Semeni papa hapa mbele ya wananchi wote wa Shekemu: Lipi ni jema kwenu, kwamba watoto wote sabini wa kiume wa Yerubaali wawatawale au mtoto mmoja? Kumbukeni kuwa mimi ni damu yenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Semeni masikioni mwao wote walio wenyeji wa Sikemu: Lililo jema lenu ni lipi? Watu 70 walio wote wana wa Yerubaali wawatawale, au awatawale mtu mmoja? Tena kumbukeni, ya kuwa huyu ni mwenzenu kwa mifupa na kwa nyama za mwili wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya, neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Museme hapa hapa mbele ya wanainchi wote wa Sekemu: Jambo gani ni jema kwenu, kwamba watoto wote makumi saba wa kiume wa Yerubali wawatawale au mutoto mumoja? Mukumbuke kwamba mimi ni damu yenu.”