Judges 9:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Shekemu waliweka washambulizi wamwotee Abimeleki kutoka vilele vya mlima. Watu hao waliwanyanganya mali zao wote waliopita huko. Abimeleki akaambiwa mambo hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo, kutokana na uadui juu yake, wenyeji wa Shekemu wakaweka watu wa kumvizia katika vilele vya milima. Wakawanyang’anya watu wote waliopita karibu nao, nayo haya yakaarifiwa kwa Abimeleki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu wa Shekemu wakaweka watu kumvizia juu ya vilele vya milima, ambao waliwanyang'anya vitu vyao watu wote waliopita njia hiyo karibu nao; naye Abimeleki aliambiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Shekemu waliweka washambulizi wamwotee Abimeleki kutoka vilele vya mlima. Watu hao waliwanyang'anya mali zao wote waliopita huko. Abimeleki akaambiwa mambo hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo, kutokana na uadui juu yake watu wa Shekemu wakaweka watu wa kumvizia katika vilele vya milima. Wakawanyang'anya watu wote waliopita karibu nao, nayo haya yakaarifiwa kwa Abimeleki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo, kutokana na uadui juu yake watu wa Shekemu wakaweka watu wa kumvizia katika vilele vya milima. Wakawanyang’anya watu wote waliopita karibu nao, nayo haya yakaarifiwa kwa Abimeleki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu wa Shekemu wakaweka watu kumvizia juu ya vilele vya milima, ambao waliwapora watu wote waliopita njia hiyo karibu nao; naye Abimeleki aliarifiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Shekemu waliweka washambulizi wamwotee Abimeleki kutoka vilele vya mlima. Watu hao waliwanyanganya mali zao wote waliopita huko. Abimeleki akaambiwa mambo hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtakia mabaya wenyeji wa Sikemu wakaweka washambuliaji juu ya milima, wawanyang'anye mali zao wote waliopita njiani hapo, walipokuwa. Naye Abimeleki akapashwa habari hizi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu wa Shekemu wakaweka watu kumvizia juu ya vilele vya milima, ambao waliwanyang’anya vitu vyao watu wote waliopita njia hiyo karibu nao; naye Abimeleki aliambiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Sekemu waliweka washambulizi wamuvizie Abimeleki kutoka vilele vya mulima. Watu hao waliwanyanganya mali zao wote waliopita kule. Abimeleki alipata habari hii.