Judges 9:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara jua litakapotoka wakati wa asubuhi, ushambulie mji. Gaali akitoka pamoja na watu wake kuja kukukabili, uwatendee ifaavyo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Gaali na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha itakuwa, asubuhi, mara litakapokucha jua, wewe utaamka asubuhi na mapema, na kuushambulia mji huo; tena, angalia, hapo yeye na wale watu walio pamoja naye watakapokutokea nje kupigana nawe, ndipo utapata kuwatenda kama utakavyopata nafasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara jua litakapotoka wakati wa asubuhi, ushambulie mji. Gaali akitoka pamoja na watu wake kuja kukukabili, uwatendee ifaavyo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Wakati yeye na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Wakati yeye na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha asubuhi na mapema, mara tu baada ya jua kuchomoza, inuka na uushambulie mji huo; na Gaali na wale watu walio pamoja naye watakapotokeza nje kupigana nawe, ndipo utakapowatenda kama utakavyoweza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara jua litakapotoka wakati wa asubuhi, ushambulie mji. Gaali akitoka pamoja na watu wake kuja kukukabili, uwatendee ifaavyo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena asubuhi, jua litakapokucha, ujidamke, uushambulie mji huu! Hapo utakapomwona, akikutokea yeye pamoja nao wote walioko kwake, utamfanyizia, mkono wako utakayoyaona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha itakuwa, asubuhi, mara litakapokucha jua, wewe utaamka asubuhi na mapema, na kuushambulia mji huo; tena, angalia, hapo yeye na wale watu walio pamoja naye watakapokutokea nje kupigana nawe, ndipo utapata kuwatenda kama utakavyopata nafasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara jua litakapotoka wakati wa asubui, ushambulie muji. Gali akitoka pamoja na watu wake kuja kupigana nawe, uwatendee sawa unavyoweza.”