Judges 9:43 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akachukua watu wake akawagawa katika vikosi vinne, ili waende kuvizia mashambani. Alipowaona watu wanatoka mjini, akatoka alikojificha akawaua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziaji huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akawatwaa watu wake, na kuwagawanya wawe vikosi vitatu, nao wakavizia mashambani; naye akaangalia, na tazama, watu walikuwa watoka humo mjini; basi akainuka na kupigana nao, akawapiga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akachukua watu wake akawagawa katika vikosi vinne, ili waende kuvizia mashambani. Alipowaona watu wanatoka mjini, akatoka alikojificha akawaua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziao huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziao huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawatwaa watu wake, na kuwagawanya katika vikosi vitatu, nao wakavizia mashambani; naye akaangalia, alipoona watu wakitoka nje ya mji, aliwashambulia na kuwaua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akachukua watu wake akawagawa katika vikosi vinne, ili waende kuvizia mashambani. Alipowaona watu wanatoka mjini, akatoka alikojificha akawaua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawachukua watu wake, akawagawanya kuwa vikosi vitatu, akawavizia hapo shambani. Alipochungulia, mara akaona, watu wakitoka mjini, akawainukia, akawapiga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akawatwaa watu wake, na kuwagawanya wawe vikosi vitatu, nao wakavizia mashambani; naye akaangalia, na tazama, watu walikuwa watoka humo mjini; basi akainuka na kupigana nao, akawapiga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akatwaa watu wake akawagawanya katika vikundi vine, kusudi waende kuvizia katika mashamba. Alipowaona watu wanatoka katika muji, akatoka alikojificha akawaua.