Judges 9:48 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abimeleki na watu wake wakaenda mlimani Salmoni, akachukua shoka akakata tawi la mti na kuliweka begani mwake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Abimeleki akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua begani mwake. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Haraka! Fanyeni kile mmeona nikifanya!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Abimeleki akakwea kwenda kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitweka fuzini mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, Haya, mliyoniona mimi kufanya, fanyeni upesi vivyo, kama nilivyofanya mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abimeleki na watu wake wakaenda mlimani Salmoni, akachukua shoka akakata tawi la mti na kuliweka begani mwake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua mabegani. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Fanyeni kile mlichoona mimi nikifanya!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Abimeleki akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua mabegani. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Fanyeni kile mlichoona mimi nikifanya!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Abimeleki akakwea kwenda katika kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitwika begani mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, “Haya, kile mlichoona nikifanya, nanyi fanyeni vivyo hivyo haraka”.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abimeleki na watu wake wakaenda mlimani Salmoni, akachukua shoka akakata tawi la mti na kuliweka begani mwake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Abimeleki akaupanda mlima wa Salmoni yeye pamoja na watu wote waliokuwa kwake, naye Abimeleki akachukua shoka mkononi mwake, akakata matawi ya miti, akayachukua na kujitwika mabegani, akawaambia wale watu waliokuwa naye: Mtakayoyaona, ya kuwa nimeyafanya, yafanyeni nanyi upesi kama mimi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Abimeleki akakwea kwenda kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitweka fuzini mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, Haya, mliyoniona mimi kufanya, fanyeni upesi vivyo, kama nilivyofanya mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abimeleki na watu wake wakaenda kwenye mulima Salmoni, akatwaa shoka, akakata tawi la muti na kuliweka juu ya bega lake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya.