Judges 9:49 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mmoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakachukua matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za ngome, wakayatia moto na kuichoma ngome; watu wote wanaume na wanawake wapatao 1,000 waliokuwa katika mnara wa Shekemu wakafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome, na kuitia moto ili kuwachoma watu wote waliokuwa ndani. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, yamkini wanaume na wanawake elfu moja, pia wakafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu hao wote vivyo wakakata kila mtu tawi lake, wakamwandama Abimeleki, wakayaweka hayo matawi pale ngomeni, na kuiteketeza moto hiyo ngome juu yao; basi hivyo watu wote wa hiyo buruji ya Shekemu wakafa, walipata kama watu elfu, waume kwa wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mmoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakachukua matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za ngome, wakayatia moto na kuichoma ngome; watu wote wanaume na wanawake wapatao 1,000 waliokuwa katika mnara wa Shekemu wakafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome na kuitia moto ili kuwachoma wale watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, karibia watu 1,000 waume kwa wake, pia wakafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome na kuitia moto ili kuwachoma wale watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, karibia watu 1,000 waume kwa wake, pia wakafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu hao wote wakakata kila mtu tawi lake, wakamfuata Abimeleki, wakayaweka hayo matawi pale ngomeni, na kuiteketeza moto hiyo ngome juu yao; ndipo watu wote wa huo mnara wa Shekemu wakafa, watu wapatao elfu moja, wanaume kwa wanawake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mmoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakachukua matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za ngome, wakayatia moto na kuichoma ngome; watu wote wanaume na wanawake wapatao 1,000 waliokuwa katika mnara wa Shekemu wakafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nao watu wote wakakata matawi wakimfuata Abimeleki, wakayaweka juu ya lile shimo, wakayachoma moto juu yao waliomo shimoni; ndivyo, walivyokufa nao watu wote waliokaa katika mnara wa Sikemu, ni kama watu 1000 wanawaume na wanawake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu hao wote vivyo wakakata kila mtu tawi lake, wakamwandama Abimeleki, wakayaweka hayo matawi pale ngomeni, na kuiteketeza moto hiyo ngome juu yao; basi hivyo watu wote wa hiyo buruji ya Shekemu wakafa, walipata kama watu elfu, waume kwa wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mumoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakabeba matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za chumba kile, wakayatia moto na kuchoma chumba. Watu wote wanaume na wanawake yapata elfu moja waliokuwa katika munara wa Sekemu wakakufa.