Judges 9:51 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kulikuwa na mnara imara katikati ya mji. Basi, wakazi wote wa mji huo wanaume na wanawake wakakimbilia humo na kujifungia ndani. Wakapanda kwenye paa la mnara huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, ndani ya huo mji kulikuwa na mnara imara, ambako watu wote wa mji, wanaume na wanawake, walikimbilia ndani yake. Wakajifungia ndani, na kupanda juu ya paa la mnara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ndani ya huo mji palikuwa na buruji yenye nguvu, na watu wote waume na wake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao wakajifungia ndani, wakapanda paa la buruji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kulikuwa na mnara imara katikati ya mji. Basi, wakazi wote wa mji huo wanaume na wanawake wakakimbilia humo na kujifungia ndani. Wakapanda kwenye paa la mnara huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, ndani ya huo mji kulikuwa na mnara imara, ambako watu wote wa mji wanaume na wanawake, watu wote wa mji, walikimbilia ndani yake. Wakajifungia ndani yake na kupanda juu ya paa la mnara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, ndani ya huo mji kulikuwa na mnara imara, ambako watu wote wa mji wanaume na wanawake, watu wote wa mji, walikimbilia ndani yake. Wakajifungia ndani yake na kupanda juu ya paa la mnara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ndani ya huo mji palikuwa na mnara wenye nguvu, na watu wote wanaume na wanawake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao wakajifungia ndani, wakapanda juu ya paa la mnara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kulikuwa na mnara imara katikati ya mji. Basi, wakazi wote wa mji huo wanaume na wanawake wakakimbilia humo na kujifungia ndani. Wakapanda kwenye paa la mnara huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katikati ya mji palikuwa na mnara wenye nguvu; ndimo, walimokimbilia wanawaume na wanawake wote na wenyeji wote wa huo mji, wakafunga nyuma yao, wakapaa kipaani pa mnara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ndani ya huo mji palikuwa na buruji yenye nguvu, na watu wote waume na wake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao wakajifungia ndani, wakapanda paa la buruji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kulikuwa munara imara katikati ya muji. Basi, wakaaji wote wa muji huo wanaume na wanawake wakakimbilia humo na kujifungia ndani. Wakapanda kwenye paa la munara huo.