Lamentations 1:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadui wamenyosha mikono yao, wanyakue vitu vyake vyote vya thamani. Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni, watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakataza kujumuika na jumuiya ya watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa ya kipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamaniko yake yote; Maana ameona ya kuwa makafiri wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadui wamenyosha mikono yao, wanyakue vitu vyake vyote vya thamani. Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni, watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakataza kujumuika na jumuiya ya watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa yakipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa ya kipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadui wamenyosha mikono yao, wanyakue vitu vyake vyote vya thamani. Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni, watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakataza kujumuika na jumuiya ya watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye kuusonga ameukunjua mkono wake, ayachukue mema yake yote yapendezayo; kwani aliona wamizimu, wakipaingia Patakatifu pake, nawe uliwakataza, wasipaingie penye mkutano wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamaniko yake yote; Maana ameona ya kuwa makafiri wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waadui wamenyoosha mikono yao, wapate kukamata vitu vyake vyote vya bei kali. Kweli umeona watu wa mataifa wakiingia ndani ya hekalu, watu ambao Yawe aliwakataza kuingia kati kusanyiko lake.