Lamentations 1:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Enyi wapita njia, hivi hamjali kitu? Tazameni! Hakuna aliyepatwa na uchungu kama mimi, uchungu alioniletea Mwenyezi-Mungu, siku ya hasira yake kali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando? Angalieni kote mwone. Je, kuna maumivu kama maumivu yangu yale yaliyotiwa juu yangu, yale Mwenyezi Mungu aliyoyaleta juu yangu katika siku ya hasira yake kali?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo Bwana amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Enyi wapita njia, hivi hamjali kitu? Tazameni! Hakuna aliyepatwa na uchungu kama mimi, uchungu alioniletea Mwenyezi-Mungu, siku ya hasira yake kali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando? Angalieni kote muone. Je, kuna maumivu kama maumivu yangu yale yaliyotiwa juu yangu, yale BWANA aliyoyaleta juu yangu katika siku ya hasira yake kali?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando? Angalieni kote mwone. Je, kuna maumivu kama maumivu yangu yale yaliyotiwa juu yangu, yale bwana aliyoyaleta juu yangu katika siku ya hasira yake kali?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Enyi wapita njia, hivi hamjali kitu? Tazameni! Hakuna aliyepatwa na uchungu kama mimi, uchungu alioniletea Mwenyezi-Mungu, siku ya hasira yake kali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Ninyi nyote mpitao njia, haviingii mioyoni mwenu? Chungulieni, mwone, kama yako maumivu yaliyo sawa nayo yangu yaliyonipata mimi, maana nimetiwa majonzi na Bwana, makali yalipomwaka moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi wapita njia wote, hivi hamujali kitu? Muangalie, muone kama kuna aliyepatwa na uchungu kama mimi, uchungu Yawe alioniletea siku ya hasira yake kali.