Lamentations 1:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nainyosha mikono yangu lakini hakuna wa kunifariji. Mwenyezi-Mungu ametoa amri dhidi yangu mimi Yakobo, jirani zangu wawe maadui zangu. Naam, mimi Yerusalemu nimekuwa kinyaa kwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sayuni ananyoosha mikono yake, lakini hakuna yeyote wa kumfariji. Mwenyezi Mungu ametoa amri kwa ajili ya Yakobo kwamba majirani zake wawe adui zake; Yerusalemu umekuwa kitu najisi miongoni mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; Bwana ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nainyosha mikono yangu lakini hakuna wa kunifariji. Mwenyezi-Mungu ametoa amri dhidi yangu mimi Yakobo, jirani zangu wawe maadui zangu. Naam, mimi Yerusalemu nimekuwa kinyaa kwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sayuni ananyosha mikono yake, lakini hakuna ye yote wa kumfariji. BWANA ametoa amri kwa ajili ya Yakobo kwamba majirani zake wawe adui zake; Yerusalemu umekuwa kitu najisi miongoni mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sayuni ananyoosha mikono yake, lakini hakuna yeyote wa kumfariji. bwana ametoa amri kwa ajili ya Yakobo kwamba majirani zake wawe adui zake; Yerusalemu umekuwa kitu najisi miongoni mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; BWANA ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nainyosha mikono yangu lakini hakuna wa kunifariji. Mwenyezi-Mungu ametoa amri dhidi yangu mimi Yakobo, jirani zangu wawe maadui zangu. Naam, mimi Yerusalemu nimekuwa kinyaa kwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sioni unainyosha mikono yake, lakini hakuna anayeutuliza moyo Bwana amewaagiza wamzungukao Yakobo, wamsonge tu; ndipo, Yerusalemu ulipowaziwa kwao kuwa si kitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; BWANA ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninainyoosha mikono yangu lakini hakuna wa kunifariji. Yawe ametoa amri juu yangu mimi Yakobo, wajirani zangu wakuwe waadui zangu. Kweli, mimi Yerusalema nimekuwa kitu kichafu kwao.