Lamentations 1:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unasononeka kwani nimekuasi vibaya. Huko nje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Angalia, Ee Mwenyezi Mungu, jinsi nilivyo katika dhiki! Nina maumivu makali ndani yangu, nami ninahangaika moyoni mwangu, kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. Huko nje, upanga unaua watu, ndani, kipo kifo tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalia, Ee Bwana; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga hufisha watu; Nyumbani mna kama mauti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unasononeka kwani nimekuasi vibaya. Huko nje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Angalia, Ee BWANA, jinsi nilivyo katika dhiki! Nina maumivu makali ndani yangu, nami ninahangaika moyoni mwangu, kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. Huko nje, upanga unaua watu, ndani, kipo kifo tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Angalia, Ee bwana, jinsi nilivyo katika dhiki! Nina maumivu makali ndani yangu, nami ninahangaika moyoni mwangu, kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. Huko nje, upanga unaua watu, ndani, kipo kifo tu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga huua watu; Nyumbani mna kama mauti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unasononeka kwani nimekuasi vibaya. Huko nje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, Bwana! Kwani nimesongeka: matumbo yangu yamechafuka, moyo wangu nao humu kifuani umepinduliwa, kwa kuwa nalikataa kukutii kabisa. Nje upanga unawaua watoto, nyumbani huwa kama mwake kifo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga hufisha watu; Nyumbani mna kama mauti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ona, ee Yawe, ninavyokuwa tabani. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unaugua maana nimekuasi vibaya. Kule inje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.