Lamentations 1:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sikiliza ninavyopiga kite; hakuna wa kunifariji. Maadui zangu wote wamesikia juu ya taabu yangu: Wanafurahi kwamba umeniletea maafa. Uifanye ile siku uliyoahidi ifike, uwafanye nao wateseke kama mimi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu, lakini hakuna yeyote wa kunifariji. Adui zangu wote wamesikia kuhusu dhiki yangu, wanafurahia lile ulilolitenda. Naomba uilete siku uliyoitangaza ili wawe kama mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sikiliza ninavyopiga kite; hakuna wa kunifariji. Maadui zangu wote wamesikia juu ya taabu yangu: wanafurahi kwamba umeniletea maafa. Uifanye ile siku uliyoahidi ifike, uwafanye nao wateseke kama mimi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu, lakini hakuna ye yote wa kunifariji. Adui zangu wote wamesikia juu ya dhiki yangu, wanafurahia lile ulilolitenda. Naomba uilete siku uliyoitangaza ili wawe kama mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu, lakini hakuna yeyote wa kunifariji. Adui zangu wote wamesikia juu ya dhiki yangu, wanafurahia lile ulilolitenda. Naomba uilete siku uliyoitangaza ili wawe kama mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sikiliza ninavyopiga kite; hakuna wa kunifariji. Maadui zangu wote wamesikia juu ya taabu yangu: Wanafurahi kwamba umeniletea maafa. Uifanye ile siku uliyoahidi ifike, uwafanye nao wateseke kama mimi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakasikia, nilivyougua, lakini hakuna anitulizaye moyo, adui zangu wote walipoyasikia mabaya yaliyonipata, wakayafurahia, ya kuwa ndiyo, uliyoyafanya wewe. Utaileta ile siku, uliyoitangaza, ndipo, watakapokuwa kama mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sikiliza ninavyolalamika; hakuna wa kunifariji. Waadui zangu wote wamesikia juu ya taabu yangu: wanafurahi kwamba umeniletea hasara. Uifanye ile siku uliyoahidi ifike, uwafanye nao wateseke kama mimi.