Lamentations 1:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukiwa sasa magofu matupu, Yerusalemu wakumbuka fahari yake. Ulipoangukia mikononi mwa maadui zake, hakuna aliyekuwako kuusaidia. Washindi wake walichekelea kuanguka kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku za mateso yake na kutangatanga, Yerusalemu hukumbuka hazina zote ambazo zilikuwa zake siku za kale. Watu wake walipoanguka katika mikono ya adui, hapatakuwa na yeyote wa kumsaidia. Watesi wake walimtazama na kumcheka katika maangamizi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamaniko yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukiwa sasa magofu matupu, Yerusalemu wakumbuka fahari yake. Ulipoangukia mikononi mwa maadui zake, hakuna aliyekuwako kuusaidia. Washindi wake walichekelea kuanguka kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku za mateso yake na kutangatanga Yerusalemu hukumbuka hazina zote ambazo zilikuwa zake katika siku za kale. Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui, hapakuwepo na ye yote wa kumsaidia. Watesi wake walimtazama na kumcheka katika maangamizi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku za mateso yake na kutangatanga, Yerusalemu hukumbuka hazina zote ambazo zilikuwa zake siku za kale. Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui, hapakuwepo na yeyote wa kumsaidia. Watesi wake walimtazama na kumcheka katika maangamizi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamanio yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukiwa sasa magofu matupu, Yerusalemu wakumbuka fahari yake. Ulipoangukia mikononi mwa maadui zake, hakuna aliyekuwako kuusaidia. Washindi wake walichekelea kuanguka kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizi za ukiwa na za kutangatanga Yerusalemu unayakumbuka mema yake yote yaliyoupendeza, ambayo ulikuwa nayo siku za kale. Watu wake walipotiwa mkononi mwake aliyewasonga, mwenye kuwasaidia hakuwako kabisa; waliowasonga walipoviona, wakacheka, jinsi walivyokomeshwa
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamaniko yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unapokuwa sasa mabomoko matupu, Yerusalema unakumbuka utukufu wake. Ulipoangukia katika mikono ya waadui zake, hakuna aliyekuwa pale kwa kuusaidia. Washindi wake walichekelea kuanguka kwake.