Lamentations 1:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uchafu wake ulionekana waziwazi, lakini wenyewe haukujali mwisho wake. Anguko lake lilikuwa kubwa mno; hakuna awezaye kuufariji. Wasema: “Tazama ee Mwenyezi-Mungu mateso yangu, maana adui yangu ameshinda.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uchafu wake umegandamana na nguo zake; hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye. Anguko lake lilikuwa la kushangaza, hapakuwa na yeyote wa kumfariji. “Tazama, Ee Mwenyezi Mungu, teso langu, kwa maana adui ameshinda.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, Bwana, teso langu; Maana huyo adui amejitukuza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uchafu wake ulionekana waziwazi, lakini wenyewe haukujali mwisho wake. Anguko lake lilikuwa kubwa mno; hakuna awezaye kuufariji. Wasema: “Tazama ee Mwenyezi-Mungu mateso yangu, maana adui yangu ameshinda.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uchafu wake umegandamana na nguo zake; hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye. Anguko lake lilikuwa la kushangaza, hapakuwepo na ye yote wa kumfariji. “Tazama, Ee BWANA, teso langu, kwa maana adui ameshinda.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uchafu wake umegandamana na nguo zake; hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye. Anguko lake lilikuwa la kushangaza, hapakuwepo na yeyote wa kumfariji. “Tazama, Ee bwana, teso langu, kwa maana adui ameshinda.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uchafu wake ulionekana waziwazi, lakini wenyewe haukujali mwisho wake. Anguko lake lilikuwa kubwa mno; hakuna awezaye kuufariji. Wasema: “Tazama ee Mwenyezi-Mungu mateso yangu, maana adui yangu ameshinda.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uchafu wake umezishika nguo zake ndefu, haukukumbuka mwisho kama huu; hivyo ulivyobwagwa chini unastaajaabisha, tena hakuna anayeutuliza moyo. E Bwana, utazame ukiwa wangu! Kwani adui wanajikuza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, teso langu; Maana huyo adui amejitukuza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uchafu wake ulionekana waziwazi, lakini muji wenyewe haukujali mwisho wake. Anguko lake lilikuwa kubwa sana; hakuna anayeweza kuufariji. Unasema: Angalia, ee Yawe, mateso yangu, maana adui yangu ameshinda.