Lamentations 2:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazee wa Siyoni wameketi chini kimya, wamejitia mavumbi vichwani na kuvaa mavazi ya gunia. Wasichana wa Yerusalemu wameinamisha vichwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazee wa Binti Sayuni wanaketi chini kimya, wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao na kuvaa gunia. Wanawali wa Yerusalemu wameinamisha vichwa vyao hadi chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wazee wa binti Sayuni huketi chini, Hunyamaza kimya; Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao, Wamejivika viunoni nguo za magunia; Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyao Kuielekea nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazee wa Siyoni wameketi chini kimya, wamejitia mavumbi vichwani na kuvaa mavazi ya gunia. Wasichana wa Yerusalemu wameinamisha vichwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazee wa Binti Sayuni wanaketi chini kimya, wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao na kuvaa nguo za gunia. Wanawali wa Yerusalemu wamesujudu hadi ardhini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazee wa Binti Sayuni wanaketi chini kimya, wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao na kuvaa nguo za gunia. Wanawali wa Yerusalemu wamesujudu hadi ardhini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wazee wa binti Sayuni huketi chini, Hunyamaza kimya; Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao, Wamejivika viunoni nguo za magunia; Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyao Kuielekea nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazee wa Siyoni wameketi chini kimya, wamejitia mavumbi vichwani na kuvaa mavazi ya gunia. Wasichana wa Yerusalemu wameinamisha vichwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazee wake binti Sioni hukaa chini na kunyamaza kimya, hujitupia mavumbi vichwani na kujifunga magunia, wanawali wa Yerusalemu huvielekeza vichwa vyao chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wazee wa binti Sayuni huketi chini, Hunyamaza kimya; Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao, Wamejivika viunoni nguo za magunia; Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyao Kuielekea nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazee wa Sayuni wameikaa chini kimya, wamejitia mavumbi juu ya vichwa na kuvaa gunia. Wabinti wa Yerusalema wameinamisha vichwa chini.