Lamentations 2:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanawalilia mama zao: “Wapi chakula, wapi kinywaji?” Huku wanazirai kama majeruhi katika barabara za mjini, na kukata roho mikononi mwa mama zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanawaambia mama zao, “Wapi mkate na divai?” wazimiapo kama watu waliojeruhiwa katika barabara za mji, maisha yao yadhoofikavyo mikononi mwa mama zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wao huwauliza mama zao, Zi wapi nafaka na divai? Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwa Katika mitaa ya mji, Hapo walipomiminika nafsi zao Vifuani mwa mama zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanawalilia mama zao: “Wapi chakula, wapi kinywaji?” huku wanazirai kama majeruhi katika barabara za mjini, na kukata roho mikononi mwa mama zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanawaambia mama zao, “Wapi mkate na divai?” Wazimiapo kama watu waliojeruhiwa katika barabara za mji, maisha yao yadhoofikavyo mikononi mwa mama zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanawaambia mama zao, “Wapi mkate na divai?” wazimiapo kama watu waliojeruhiwa katika barabara za mji, maisha yao yadhoofikavyo mikononi mwa mama zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wao huwauliza mama zao, Ziko wapi nafaka na divai? Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwa Katika mitaa ya mji, Hapo walipomiminika nafsi zao Vifuani mwa mama zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanawalilia mama zao: “Wapi chakula, wapi kinywaji?” Huku wanazirai kama majeruhi katika barabara za mjini, na kukata roho mikononi mwa mama zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao huwauliza mama zao: Mikate na mvinyo iko wapi? wanapozimia barabarani mjini kama wenye kupigwa kwa panga, au wanapokata roho vifuani kwa mama zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wao huwauliza mama zao, Zi wapi nafaka na divai? Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwa Katika mitaa ya mji, Hapo walipomiminika nafsi zao Vifuani mwa mama zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanawalilia wamama zao: Chakula kiko wapi, kinywaji kiko wapi? Wanazimia kama wale walioumizwa katika barabara za muji, na kukata roho katika mikono ya wamama zao.