Lamentations 2:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu, hawakufichua wazi uovu wako ili wapate kukurekebisha, bali walikuonea kauli ya uongo na ya kupotosha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maono ya manabii wako yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, hawakuifunua dhambi yako ili kukuzuilia kwenda utumwani. Maneno waliyokupa yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu, hawakufichua wazi uovu wako ili wapate kukurekebisha, bali walikuonea kauli ya uongo na ya kupotosha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maono ya manabii wako yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, hawakuifunua dhambi yako katika kuzuilia kwenda kwako utumwani. Maneno waliyokupa yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maono ya manabii wako yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, hawakuifunua dhambi yako ili kukuzuilia kwenda utumwani. Maneno waliyokupa yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu, hawakufichua wazi uovu wako ili wapate kukurekebisha, bali walikuonea kauli ya uongo na ya kupotosha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafumbuaji wako waliyoyaona yalikuwa uwongo na upumbavu, hawakuyafunua maovu yako, uliyoyafanya, wayafungue mafungo yako, ila walipokuambia: Tumeona, yalikuwa uwongo, wakupatie kutekwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu. Hawakufichua wazi uovu wako kusudi wapate kukurudishia hali yako ya mbele. Lakini walikuonea maono ya uongo na ya kupotosha.