Lamentations 2:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maiti za vijana na wazee zimelala vumbini barabarani, wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa upanga; umewaua bila huruma siku ya hasira yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wasichana wangu na wavulana wangu wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maiti za vijana na wazee zimelala vumbini barabarani, wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa upanga; umewaua bila huruma siku ya hasira yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wavulana wangu na wasichana wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wavulana wangu na wasichana wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maiti za vijana na wazee zimelala vumbini barabarani, wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa upanga; umewaua bila huruma siku ya hasira yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa wazee hulala barabarani chini, wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa panga; umewaua siku ile, makali yako yalipotokea, ukawachinja pande zote pasipo kuwaonea uchungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maiti za vijana na wazee zimelala ndani ya mavumbi katika barabara, wabinti na vijana wangu wameuawa kwa upanga; umewaua bila huruma siku ya hasira yako.