Lamentations 2:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amevuta upinde wake kama adui, na kuuweka mkono wake wa kulia tayari, amewaua wote tuliowaonea fahari katika maskani yetu watu wa Siyoni. Ametumiminia hasira yake kama moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ameupinda upinde wake kama adui, mkono wake wa kuume uko tayari. Kama vile adui amewaua wote waliokuwa wanapendeza jicho, amemwaga ghadhabu yake kama moto juu ya hema la Binti Sayuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kuume kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina kani yake kama moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amevuta upinde wake kama adui, na kuuweka mkono wake wa kulia tayari, amewaua wote tuliowaonea fahari katika maskani yetu watu wa Siyoni. Ametumiminia hasira yake kama moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ameupinda upindi wake kama adui, mkono wake wa kuume uko tayari. Kama vile adui amewachinja wote waliokuwa wanapendeza jicho, amemwaga ghadhabu yake kama moto juu ya hema la Binti Sayuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ameupinda upinde wake kama adui, mkono wake wa kuume uko tayari. Kama vile adui amewachinja wote waliokuwa wanapendeza jicho, amemwaga ghadhabu yake kama moto juu ya hema la Binti Sayuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina ghadhabu yake kama moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amevuta upinde wake kama adui, na kuuweka mkono wake wa kulia tayari, amewaua wote tuliowaonea fahari katika maskani yetu watu wa Siyoni. Ametumiminia hasira yake kama moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaupinda upindi wake, akawa kama adui, akajipanga na kuutumia mkono wake wa kuume, kama mwenye kusonga, akawaua wote walipendeza macho; hemani mwake binti Sioni ndimo, alimoyaeneza makali yake kama moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kuume kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina kani yake kama moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amevuta upinde wake kama adui, na kuuweka mukono wake wa kuume tayari, amewaua wote waliopendeza macho. Amemwanga hasira yake kama moto katika hema yetu watu wa Sayuni.