Lamentations 2:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini, maskani yake ameiharibu. Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni, kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. Mwenyezi Mungu amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; Bwana amezisahauzisha katika Sayuni Sikukuu za makini na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini, maskani yake ameiharibu. Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni, kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. BWANA amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewakataa kwa dharau mfalme na kuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. bwana amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; BWANA amezisahaulisha katika Sayuni Sikukuu na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini, maskani yake ameiharibu. Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni, kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akakivunja kitalu chake kama cha bustanini, akauangamiza ua wake uliokuwa wa kukusanyikia; kisha Bwana akawasahaulisha Wasioni sikukuu nazo za mapumziko, akamtupa mfalame na mtambikaji, makali yake yalipowapatiliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; BWANA amezisahauzisha katika Sayuni Sikukuu za makini na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amelibomoa hekalu lake kama kibanda katika bustani, ameharibu pahali pake pa kusanyiko. Amefanya sikukuu na siku ya Sabato visahauliwe kule Sayuni, kwa hasira yake kubwa amewakataa mufalme na makuhani.