Lamentations 2:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ameipuuza madhabahu yake na hekalu lake amelikataa. Kuta za majumba mjini amewaachia maadui wazibomoe, wakapiga kelele humo nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu kama kelele za wakati wa sikukuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana amekataa madhabahu yake na kuacha mahali patakatifu pake. Amemkabidhi adui kuta za majumba yake ya kifalme; wameshangilia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake, Amepachukia patakatifu pake; Amezitia katika mikono ya hao adui Kuta za majumba yake; Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya Bwana Kama katika siku ya kusanyiko la makini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ameipuuza madhabahu yake na hekalu lake amelikataa. Kuta za majumba mjini amewaachia maadui wazibomoe, wakapiga kelele humo nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu kama kelele za wakati wa sikukuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana amekataa madhabahu yake na kuacha mahali patakatifu pake. Amemkabidhi adui kuta za majumba yake ya kifalme; wamepiga kelele katika nyumba ya BWANA kama katika siku ya sikukuu iliyoamuriwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana amekataa madhabahu yake na kuacha mahali patakatifu pake. Amemkabidhi adui kuta za majumba yake ya kifalme; wamepiga kelele katika nyumba ya bwana kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake, Amepachukia patakatifu pake; Amezitia katika mikono ya hao adui Kuta za majumba yake; Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANA Kama katika sikukuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ameipuuza madhabahu yake na hekalu lake amelikataa. Kuta za majumba mjini amewaachia maadui wazibomoe, wakapiga kelele humo nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu kama kelele za wakati wa sikukuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pake pa kutambikiwa Bwana akapaona kuwa pabaya, napo Patakatifu pake, akapaacha. Akazitia mikononi mwa adui kuta za majumba yake, wakapiga makelele Nyumbani mwa Bwana kama yale ya sikukuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake, Amepachukia patakatifu pake; Amezitia katika mikono ya hao adui Kuta za majumba yake; Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANA Kama katika siku ya kusanyiko la makini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe amechukia mazabahu yake na hekalu lake amelikataa. Amewaachilia waadui wazibomoe kuta za nyumba zake katika muji. Wakapiga kelele ndani ya nyumba ya Yawe kama kelele za wakati wa sikukuu.