Lamentations 4:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jinsi gani dhahabu yetu ilivyochujuka, dhahabu safi kabisa ilivyobadilika! Mawe ya thamani yametawanywa yamesambaa barabarani kote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jinsi dhahabu ilivyopoteza mng’ao wake, dhahabu iliyo safi haing’ai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jinsi dhahabu ilivyoacha kung'aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jinsi gani dhahabu yetu ilivyochujuka, dhahabu safi kabisa ilivyobadilika! Mawe ya thamani yametawanywa yamesambaa barabarani kote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jinsi dhahabu ilivyopoteza mng'ao wake, dhahabu iliyo safi imekuwa haing'ai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jinsi dhahabu ilivyopoteza mng’ao wake, dhahabu iliyo safi haing’ai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jinsi dhahabu ilivyoacha kung'aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jinsi gani dhahabu yetu ilivyochujuka, dhahabu safi kabisa ilivyobadilika! Mawe ya thamani yametawanywa yamesambaa barabarani kote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Imekuwaje, dhahabu ikichujuka, dhahabu iliyo nzuri yenyewe ikigeuka kuwa mbaya? Imekuwaje, vijiwe vya pambo vya Patakatifu vikitupwa pembeni penye barabara zote?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jinsi dhahabu ilivyoacha kung’aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Namna gani zahabu yetu ilivyochakaa, zahabu safi kabisa ilivyobadilika! Mawe ya bei kali yamesambazwa kwa barabara zote.