Lamentations 4:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea, yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu, yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi wake tutaishi miongoni mwa mataifa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu, pumzi ya uhai wetu hasa, alinaswa katika mitego yao. Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake tungeishi miongoni mwa mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea, yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu, yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi wake tutaishi miongoni mwa mataifa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpakwa mafuta wa BWANA, pumzi ya uhai wetu hasa, alinaswa katika mitego yao. Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpakwa mafuta wa bwana, pumzi ya uhai wetu hasa, alinaswa katika mitego yao. Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea, yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu, yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi wake tutaishi miongoni mwa mataifa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliyekuwa kama pumzi puani mwetu yeye aliyepakwa mafuta na Bwana akanaswa katika mashimo yao; ni yeye, tuliyemsema: Kivulini kwake tutakaa kwenye makabila ya watu
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walimunasa yule ambaye maisha yetu yalimutegemea, yule mufalme aliyechaguliwa na Yawe yule ambaye tulisema juu yake: Chini ya ulinzi wake tutaishi kati ya mataifa.