Leviticus 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu, mbele ya Mwenyezi-Mungu, hao makuhani, wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu pande zake zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za Mwenyezi Mungu, nao wana wa Haruni walio makuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za Bwana; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu, mbele ya Mwenyezi-Mungu, hao makuhani, wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu pande zake zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atamchinja upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za BWANA, nao wana wa Aroni kuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za bwana, nao wana wa Haruni walio makuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za BWANA; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu, mbele ya Mwenyezi-Mungu, hao makuhani, wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu pande zake zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amchinje mbele ya Bwana kando ya meza ya kutambikia upande wake wa kaskazini, nayo damu yake wana wa Haroni walio watambikaji na wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za BWANA; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atamuchinjia upande wa kaskazini wa mazabahu, mbele ya Yawe, hao makuhani wazao wa Haruni watainyunyizia mazabahu damu pande zake zote.