Leviticus 1:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Mwenyezi Mungu, kisha wana wa Haruni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Bwana; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atamchinja yule fahali mchanga mbele za BWANA, kisha wana wa Aroni kuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu iliyoko penye ingilio la Hema la Kukutania.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atamchinja yule fahali mchanga mbele za bwana, kisha wana wa Haruni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele za BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha amchinje huyo mwana wa ng'ombe mbele ya Bwana, nao wana wa Haroni walio watambikaji na waipeleke damu, nayo hiyo damu wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia iliyopo hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atamchinja huyo ng’ombe mbele ya BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, atamuchinja huyo ngombe mbele ya Yawe. Nao makuhani wazao wa Haruni wataichukua damu na kuinyunyizia mazabahu inayokuwa kwenye mulango wa hema la mukutano, pande zake zote.