Leviticus 10:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao Nadabu na Abihu, wanawe Aroni, walichukua kila mmoja chetezo chake, wakaweka moto na ubani, wakamtolea Mwenyezi-Mungu moto najisi, ambao haukulingana na agizo lake Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea Mwenyezi Mungu moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao Nadabu na Abihu, wanawe Aroni, walichukua kila mmoja chetezo chake, wakaweka moto na ubani, wakamtolea Mwenyezi-Mungu moto najisi, ambao haukulingana na agizo lake Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nadabu na Abihu wana wa Aroni wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea BWANA moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea bwana moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto najisi mbele za BWANA, ambao yeye hakuwaagiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao Nadabu na Abihu, wanawe Aroni, walichukua kila mmoja chetezo chake, wakaweka moto na ubani, wakamtolea Mwenyezi-Mungu moto najisi, ambao haukulingana na agizo lake Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Haroni, Nadabu na Abihu, wakachukua kila mtu chetezo chake, wakavitia moto, wakaweka mavukizo juu yake, wakamtolea Bwana moto huu mgeni, Bwana asiowaagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya BWANA, ambao yeye hakuwaagiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mumoja chetezo chake, wakaweka moto na ubani, wakamutolea Yawe moto usioruhusiwa, ambao haukulingana na agizo la Yawe.