Leviticus 10:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kidari ambacho hufanywa nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu na mguu unaotolewa sadaka kama ishara, mnaweza kula mahali popote pasipo najisi. Utakula wewe, na watoto wako wa kiume na wa kike. Vitu hivyo umepewa kama haki yako na ya wazawa wako kutoka sadaka za amani za watu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila katika mahali patakatifu; mmepewa wewe na wanao kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kidari ambacho hufanywa nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu na mguu unaotolewa sadaka kama ishara, mnaweza kula mahali popote pasipo najisi. Utakula wewe, na watoto wako wa kiume na wa kike. Vitu hivyo umepewa kama haki yako na ya wazawa wako kutoka sadaka za amani za watu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila mahali safi pa kawaida ya ibada; mmepewa wewe na watoto wako kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila mahali safi pa kawaida ya ibada; mmepewa wewe na watoto wako kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kidari ambacho hufanywa nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu na mguu unaotolewa sadaka kama ishara, mnaweza kula mahali popote pasipo najisi. Utakula wewe, na watoto wako wa kiume na wa kike. Vitu hivyo umepewa kama haki yako na ya wazawa wako kutoka sadaka za amani za watu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vidari vilivyopitishwa motoni na mapaja yaliyonyanyuliwa hayo mtayala mahali panapotakata, wewe na wanao wa kiume na wa kike, kwani hii ni haki yako na ya wanao, yatolewe katika ng'ombe za tambiko za shukrani za wana wa Isiraeli, myapate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kilali ambacho wanafanya nacho kitambulisho cha kumutolea Yawe na muguu unaotolewa sadaka kama vile kitambulisho, munaweza kuvikulia pahali popote pasipo kuwa pachafu. Utakula wewe na watoto wako wanaume na wanawake. Vitu hivyo umepewa kama haki yako na ya wazao wako kutoka sadaka za amani za watu wa Israeli.