Leviticus 10:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ule mguu uliotolewa na kidari cha sadaka ya kufanyia ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu watavileta pamoja na sadaka za mafuta zitolewazo kwa moto, ili kufanya ishara ya kuvitolea mbele ya Mwenyezi-Mungu, viwe sadaka ya kutolewa kwa ishara. Hivyo vitakuwa vyako pamoja na wanao; ni haki yenu milele kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya wanyama wa sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako na wanao milele, kama Mwenyezi Mungu alivyoagiza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama Bwana alivyoagiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ule mguu uliotolewa na kidari cha sadaka ya kufanyia ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu watavileta pamoja na sadaka za mafuta zitolewazo kwa moto, ili kufanya ishara ya kuvitolea mbele ya Mwenyezi-Mungu, viwe sadaka ya kutolewa kwa ishara. Hivyo vitakuwa vyako pamoja na wanao; ni haki yenu milele kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele za BWANA kama sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako la kawaida na wanao, kama BWANA alivyoagiza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele za bwana kama sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako la kawaida na wanao, kama bwana alivyoagiza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama BWANA alivyoagiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ule mguu uliotolewa na kidari cha sadaka ya kufanyia ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu watavileta pamoja na sadaka za mafuta zitolewazo kwa moto, ili kufanya ishara ya kuvitolea mbele ya Mwenyezi-Mungu, viwe sadaka ya kutolewa kwa ishara. Hivyo vitakuwa vyako pamoja na wanao; ni haki yenu milele kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mapaja ya kunyanyuliwa na vidari vya kupitishwa motoni kwanza wayapeleke hapo, mafuta yanapochomwa moto, wavipitishe motoni mbele ya Bwana hivyo vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni. Kuvipata hivi itakuwa haki yako na ya wanao ya kale na kale, kama Bwana alivyoagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama BWANA alivyoagiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ule muguu uliotolewa na kilali cha sadaka ya kufanyia kitambulisho cha kumutolea Yawe watavileta pamoja na sadaka za mafuta zinazotolewa kwa moto, kwa kufanya kitambulisho cha kuvitolea mbele ya Yawe, vikuwe sadaka ya kutolewa kwa kitambulisho. Hivyo vitakuwa vyako pamoja na wana wako; ni haki yenu milele kama vile Yawe alivyoamuru.