Leviticus 10:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose alichunguza kwa makini kuhusu mbuzi mmoja aliyetolewa sadaka ya kuondoa dhambi, kumbe akagundua kuwa alikwisha teketezwa. Hivyo akawakasirikia sana Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliosalia, akawauliza,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa alipouliza kuhusu mbuzi aliyetolewa sadaka ya dhambi na kugundua kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni waliobaki. Akawauliza,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuchomwa moto; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose alichunguza kwa makini kuhusu mbuzi mmoja aliyetolewa sadaka ya kuondoa dhambi, kumbe akagundua kuwa alikwisha teketezwa. Hivyo akawakasirikia sana Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliosalia, akawauliza,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose alipouliza kuhusu mbuzi atolewaye kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kukuta kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliobaki, akawauliza,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa alipouliza kuhusu mbuzi atolewaye kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kukuta kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni waliobaki, akawauliza,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuteketezwa; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose alichunguza kwa makini kuhusu mbuzi mmoja aliyetolewa sadaka ya kuondoa dhambi, kumbe akagundua kuwa alikwisha teketezwa. Hivyo akawakasirikia sana Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliosalia, akawauliza,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alipomtafuta sana dume la mbuzi aliyetolewa kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo aliona, ya kuwa amekwisha kuteketea; ndipo, alipowakasirikia wale wana wa Haroni waliosalia, Elazari na Itamari, akawaambia:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuchomwa moto; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa akachunguza kwa uangalifu juu ya mbuzi mumoja aliyetolewa sadaka kwa ajili ya zambi, akatambua kwamba alikwisha kuteketezwa kwa moto. Hivyo akawakasirikia sana Eleazari na Itamari, wana wa Haruni waliobakia, akawauliza: