Leviticus 10:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msitoke nje ya mlango wa hema la mkutano, la sivyo mtakufa; kwani mafuta ya kupaka ya Mwenyezi-Mungu yangali juu yenu.” Aroni na wanawe wakafanya kama Mose alivyosema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta ya Mwenyezi Mungu ya upako yako juu yenu.” Hivyo wakafanya kama vile Musa alivyosema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hamtatoka nje mlangoni mwa hema ya kukutania, msije mkafa; kwa sababu mafuta ya kutiwa ya Bwana ya juu yenu. Nao wakafanya kama hilo neno la Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msitoke nje ya mlango wa hema la mkutano, la sivyo mtakufa; kwani mafuta ya kupaka ya Mwenyezi-Mungu yangali juu yenu.” Aroni na wanawe wakafanya kama Mose alivyosema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta ya BWANA ya upako yako juu yenu.” Kwa hiyo wakafanya kama vile Mose alivyosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta ya bwana ya upako yako juu yenu.” Hivyo wakafanya kama vile Musa alivyosema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hamtatoka nje mlangoni mwa hema ya kukutania, msije mkafa; kwa sababu mafuta ya kutiwa ya BWANA yako juu yenu. Nao wakafanya kama hilo neno la Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msitoke nje ya mlango wa hema la mkutano, la sivyo mtakufa; kwani mafuta ya kupaka ya Mwenyezi-Mungu yangali juu yenu.” Aroni na wanawe wakafanya kama Mose alivyosema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi msitoke hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, msife! Kwani mmekwisha kupakwa mafuta ya Bwana. Nao wakafanya, kama Mose alivyowaagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hamtatoka nje mlangoni mwa hema ya kukutania, msije mkafa; kwa sababu mafuta ya kutiwa ya BWANA ya juu yenu. Nao wakafanya kama hilo neno la Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musitoke inje ya mulango wa hema la mukutano, kama sivyo mutakufa. Maana mafuta ya kupakaa ya Yawe yangali juu yenu. Haruni na wana wake wakafanya kama vile Musa alivyosema.