Leviticus 10:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnapoingia ndani ya hema la mkutano, wewe na wanao msinywe divai wala kileo chochote, la sivyo mtakufa. Hii itakuwa sheria ya kudumu katika vizazi vyenu vyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnapoingia ndani ya hema la mkutano, wewe na wanao msinywe divai wala kileo chochote, la sivyo mtakufa. Hii itakuwa sheria ya kudumu katika vizazi vyenu vyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnapoingia ndani ya hema la mkutano, wewe na wanao msinywe divai wala kileo chochote, la sivyo mtakufa. Hii itakuwa sheria ya kudumu katika vizazi vyenu vyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mvinyo au kileo kingine usinywe wewe wala wanao, ulio nao, mkiingia Hemani mwa Mkutano, msife! Huu ndio mwiko wa kale na kale wa vizazi vyenu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munapoingia ndani ya hema la mukutano, wewe na wana wako musikunywe divai wala kileo chochote, kama sivyo mutakufa. Hili litakuwa sharti ambalo vizazi vyenu vyote wanapaswa kulifuata siku zote.