Leviticus 11:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila kitu ambacho sehemu ya mzoga imekiangukia, kitakuwa najisi. Ikiwa ni tanuri au jiko, ni lazima kivunjwe. Vitakuwa najisi navyo ni najisi kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Chochote ambacho mzoga utaangukia kitakuwa najisi. Jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila kitu ambacho sehemu ya mzoga imekiangukia, kitakuwa najisi. Ikiwa ni tanuri au jiko, ni lazima kivunjwe. Vitakuwa najisi navyo ni najisi kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Cho chote ambacho mzoga wa mmojawapo utaangukia kitakuwa najisi, jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Chochote ambacho mzoga wa mmojawapo utaangukia kitakuwa najisi. Jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande chochote cha mizoga yao kitakuwa najisi; iwe ni tanuri, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila kitu ambacho sehemu ya mzoga imekiangukia, kitakuwa najisi. Ikiwa ni tanuri au jiko, ni lazima kivunjwe. Vitakuwa najisi navyo ni najisi kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho cho chote, mzoga mmoja tu miongoni mwao utakachokiangukia, ni chenye uchafu; kama ni jiko la kuchomea mikate au la kupikia, sharti libomolewe, maana ni lenye uchafu, hata kwenu sharti liwe lenye uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila kitu ambacho sehemu ya muzoga imekiangukia, kitakuwa kichafu. Ikiwa ni furu au jiko, kinapaswa kuvunjwa. Vitakuwa vichafu navyo ni vichafu kwenu.