Leviticus 11:44 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ndimi Mungu wenu, jiwekeni wakfu na kuwa watakatifu kwa maana mimi ni mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ndimi Mungu wenu, jiwekeni wakfu na kuwa watakatifu kwa maana mimi ni mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi ndimi BWANA Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe cho chote kile kiendacho juu ya ardhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ndimi Mungu wenu, jiwekeni wakfu na kuwa watakatifu kwa maana mimi ni mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mimi ni Bwana, Mungu wenu, kwa hiyo sharti mjitakase, mwe watakatifu, kwani mimi ni mtakatifu. Msijipatie uchafu wenyewe kwao hao wadudu wote wanaotambaa juu ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu mimi ni Yawe, Mungu wenu, mujitakase na kuwa watakatifu kwa maana mimi ni mutakatifu. Wala musijichafue na kitu chochote kinachotambaa juu ya inchi.