Leviticus 12:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mama mtoto ataendelea kuwa najisi kwa muda wa siku thelathini na tatu. Wakati huo, kamwe asiguse chochote kilichowekwa wakfu wala kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakasika kwake zitakapotimia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu, ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu, hadi siku za kutakaswa kwake zimetimia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mama mtoto ataendelea kuwa najisi kwa muda wa siku thelathini na tatu. Wakati huo, kamwe asiguse chochote kilichowekwa wakfu wala kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakasika kwake zitakapotimia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu cho chote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakaswa kwake zimetimia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu, ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu, mpaka siku za kutakaswa kwake zimetimia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo mwanamke atakaa muda wa siku thelathini na tatu ili kutakata damu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mama mtoto ataendelea kuwa najisi kwa muda wa siku thelathini na tatu. Wakati huo, kamwe asiguse chochote kilichowekwa wakfu wala kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakasika kwake zitakapotimia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha huyo mwanamke na akae siku 33, damu yake ipate kutakata; cho chote kilicho kitakatifu asikiguse, wala asiingie Patakatifu, mpaka siku za weuo wake zitimie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mama wa mutoto ataendelea kuwa muchafu kwa muda wa siku makumi tatu na tatu. Wakati huo, asiguse chochote kilichotakaswa wala kuingia Pahali Patakatifu mpaka siku za kutakasika kwake zitakapotimia.