Leviticus 12:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, iwe amepata mtoto wa kiume au wa kike, atamletea kuhani mlangoni mwa hema la mkutano mwanakondoo wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa au hua, kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Siku zake za utakaso kwa ajili ya mwana au binti zitakapotimia, mwanamke huyo atamletea kuhani kwenye ingilio la Hema la Kukutania mwana-kondoo mwenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au hua kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mwana, au kwa ajili ya binti, ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, iwe amepata mtoto wa kiume au wa kike, atamletea kuhani mlangoni mwa hema la mkutano mwanakondoo wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa au hua, kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Siku zake za utakaso kwa ajili ya mwana au binti, zitakapotimia, mwanamke huyo atamletea kuhani kwenye ingilio la Hema la Kukutania mwana-kondoo mwenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa au hua kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Siku zake za utakaso kwa ajili ya mwana au binti zitakapotimia, mwanamke huyo atamletea kuhani kwenye ingilio la Hema la Kukutania mwana-kondoo mwenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au hua kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mtoto wa kiume, au kwa ajili ya mtoto wa kike ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, iwe amepata mtoto wa kiume au wa kike, atamletea kuhani mlangoni mwa hema la mkutano mwanakondoo wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa au hua, kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za weuo wake kwa kuzaa mtoto mume au mke zitakapotimia, na apeleke mwana kondoo wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima na kinda la njiwa manga au hua kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo akiwafikisha hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano kwake mtambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mwana, au kwa ajili ya binti, ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, ikuwe amepata mutoto mwanaume au mwanamuke, atamuletea kuhani kwenye mulango wa hema la mukutano mwana-kondoo wa mwaka mumoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na kitoto cha njiwa au hua, kwa ajili ya sadaka ya zambi.