Leviticus 12:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamtolea mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfanyia huyo mama ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. Hivyo huyo mwanamke atakuwa safi kutokana na damu yake. Huo ni mwongozo kuhusu mwanamke yeyote anayejifungua mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atavitoa mbele za Mwenyezi Mungu ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na kisha atatakasika kutokana na kutokwa na damu. “ ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya mwanamke atakayezaa mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na yeye atawasongeza mbele za Bwana, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika na jicho la damu yake. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, kwamba ni mtoto mume au mke.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamtolea mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfanyia huyo mama ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. Hivyo huyo mwanamke atakuwa safi kutokana na damu yake. Huo ni mwongozo kuhusu mwanamke yeyote anayejifungua mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atavitoa mbele za BWANA ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na kisha atakuwa safi kwa desturi ya ibada kutokana na kutokwa damu kwake. “ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya mwanamke atakayezaa mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atavitoa mbele za bwana ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na kisha atakuwa safi kwa desturi ya ibada kutokana na kutokwa damu kwake. “ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya mwanamke atakayezaa mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na yeye atawasongeza mbele za BWANA, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, awe ni mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamtolea mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfanyia huyo mama ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. Hivyo huyo mwanamke atakuwa safi kutokana na damu yake. Huo ni mwongozo kuhusu mwanamke yeyote anayejifungua mtoto wa kiume au wa kike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atamtolea Bwana hizo ng'ombe za tambiko na kumpatia upozi; ndipo, atakapotakata kwa ajili ya hiyo damu yake iliyomtoka. Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya mwanamke aliyezaa mtoto mume au mke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na yeye atawasongeza mbele za BWANA, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika na jicho la damu yake. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, kwamba ni mtoto mume au mke.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atamutolea mbele ya Yawe na kumufanyia huyo mama ibada ya upatanisho mbele ya Yawe. Hivyo huyo mwanamuke atakuwa safi kwa ajili ya kutokwa na damu yake. Hii ni sheria inayoelekea mwanamuke yeyote anayezaa mutoto mwanaume au mwanamuke.