Leviticus 13:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ukoma umemshika na umeenea mwili mzima, toka utosini hadi nyayoni kama atakavyoona kuhani,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ikiwa ugonjwa utakuwa umeenea kwenye ngozi yake yote kwa kadiri kuhani atakavyoweza kuona, kwamba umeenea kwenye ngozi yote ya huyo mgonjwa kutoka kichwani hadi wayo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kwamba huo ukoma ukitokeza katika ngozi yake, na ukoma ukamwenea ngozi yote, tangu kichwa hata miguuni, kama aonavyo kuhani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ukoma umemshika na umeenea mwili mzima, toka utosini hadi nyayoni kama atakavyoona kuhani,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ikiwa ugonjwa utakuwa umeenea kwenye ngozi yake yote kwa kadiri kuhani atakavyoweza kuona, kwamba umeenea kwenye ngozi yote ya huyo mgonjwa kutoka kichwani mpaka wayo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ikiwa ugonjwa utakuwa umeenea kwenye ngozi yake yote kwa kadiri kuhani atakavyoweza kuona, kwamba umeenea kwenye ngozi yote ya huyo mgonjwa kutoka kichwani mpaka wayo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huo ukoma ukitokeza katika ngozi ya mgonjwa, na ukaenea katika ngozi yake yote, kutoka kichwani hadi miguuni, kama kuhani atakavyoweza kuona,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ukoma umemshika na umeenea mwili mzima, toka utosini hadi nyayoni kama atakavyoona kuhani,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ukoma ukitokea na kuenea katika ngozi po pote, ukoma ukiifunika hiyo ngozi iliyopatwa nao toka kichwani pake huyo mtu mpaka miguuni pake pote, macho ya mtambikaji yanapotazama,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kwamba huo ukoma ukitokeza katika ngozi yake, na ukoma ukamwenea ngozi yote, tangu kichwa hata miguuni, kama aonavyo kuhani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ukoma umemushika na umeenea mwili muzima, toka kwenye kichwa mpaka kwenye miguu kama vile kuhani atakavyoona,