Leviticus 13:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamwangalia na akiona kuwa kimegeuka kuwa cheupe, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atamchunguza, na kama vidonda vimekuwa vyeupe, kuhani atamtangaza mgonjwa huyo kuwa safi; kisha atakuwa safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na huyo kuhani atamwangalia; na tazama, ikiwa hilo pigo limegeuzwa kuwa jeupe, ndipo huyo kuhani atasema kuwa yu safi huyo aliyekuwa na pigo; yeye yu safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamwangalia na akiona kuwa kimegeuka kuwa cheupe, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atamchunguza, kama vidonda vimekuwa vyeupe, kuhani atamtangaza mgonjwa huyo kuwa safi; kisha atakuwa safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atamchunguza, na kama vidonda vimekuwa vyeupe, kuhani atamtangaza mgonjwa huyo kuwa safi; kisha atakuwa safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na huyo kuhani atamwangalia; ikiwa hilo pigo limegeuzwa kuwa jeupe, ndipo huyo kuhani atasema kuwa huyo aliyekuwa na pigo ni safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamwangalia na akiona kuwa kimegeuka kuwa cheupe, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji akimtazama na kuona, ya kama hapo palipopatwa na ukoma pamegeuka kuwa peupe, mtambikaji hana budi kusema, ya kama huyu aliyepatwa na ukoma ametakata, kwa kuwa amekwisha kutakata kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na huyo kuhani atamwangalia; na tazama, ikiwa hilo pigo limegeuzwa kuwa jeupe, ndipo huyo kuhani atasema kuwa yu safi huyo aliyekuwa na pigo; yeye yu safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atamwangalia na akiona kwamba kimegeuka kuwa cheupe, basi, atamutangaza mutu yule kuwa safi.