Leviticus 13:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au kipaku mwilini mwake, ikadhihirika kwamba ni ukoma, basi, ataletwa kwa kuhani Aroni au mmoja wa wanawe aliye kuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe, au upele, au alama nyeupe juu ya ngozi yake, ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, ni lazima aletwe kwa kuhani Haruni, au kwa mmoja wa wanawe, hao makuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu atakapokuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king'aacho, nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmojawapo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au kipaku mwilini mwake, ikadhihirika kwamba ni ukoma, basi, ataletwa kwa kuhani Aroni au mmoja wa wanawe aliye kuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Iwapo mtu ye yote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, ni lazima aletwe kwa Haruni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king'aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au kipaku mwilini mwake, ikadhihirika kwamba ni ukoma, basi, ataletwa kwa kuhani Aroni au mmoja wa wanawe aliye kuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ngozi ya mwili wa mtu ikitoa kivimbe au kipele au balanga, hiyo ngozi ya mwili wake ikitaka kumpatia pigo la ukoma, na apelekwe kwa mtambikaji Haroni au kwa mmoja wao wanawe walio watambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu atakapokuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king’aacho, nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmojawapo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa mutu yeyote atakuwa na kivimba au upele au chunuku juu ya mwili wake, ikionekana kwamba ni ukoma, basi, ataletwa kwa kuhani Haruni au mumoja wa wana wake anayekuwa kuhani.