Leviticus 13:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamwangalia huyo mtu. Kuhani akiona pamegeuka kuwa na shimo na nywele za mahali hapo zimegeuka kuwa nyeupe, basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; huo ni ugonjwa wa ukoma ambao umetokana na jipu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atapachunguza, na kama uvimbe umeingia ndani ya ngozi, na nywele zimegeuka kuwa nyeupe, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza uliojitokeza pale jipu lilipokuwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kuhani ataangalia, na tazama, kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na malaika yakiwa yamegeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atasema kwamba yu najisi; ni pigo la ukoma limetokea katika hilo jipu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamwangalia huyo mtu. Kuhani akiona pamegeuka kuwa na shimo na nywele za mahali hapo zimegeuka kuwa nyeupe, basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; huo ni ugonjwa wa ukoma ambao umetokana na jipu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atapachunguza, na kama uvimbe umezama ndani ya ngozi na nywele zimegeuka kuwa nyeupe, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza uliojitokeza pale jipu lilipokuwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atapachunguza, na kama uvimbe umezama ndani ya ngozi, na nywele zimegeuka kuwa nyeupe, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza uliojitokeza pale jipu lilipokuwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kuhani ataangalia, kama kutaonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na malaika yakiwa yamegeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi; ni pigo la ukoma limetokea katika hilo jipu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamwangalia huyo mtu. Kuhani akiona pamegeuka kuwa na shimo na nywele za mahali hapo zimegeuka kuwa nyeupe, basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; huo ni ugonjwa wa ukoma ambao umetokana na jipu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji akimtazama na kuona, ya kama hapo panaonekana kuwa panabonyea katika ngozi, tena ya kama nywele zimegeuka kuwa nyeupe, mtambikaji hana budi kusema, ya kama ni mwenye uchafu, ndio ugonjwa wa ukoma uliotokea hapo penye jipu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kuhani ataangalia, na tazama, kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na malaika yakiwa yamegeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atasema kwamba yu najisi; ni pigo la ukoma limetokea katika hilo jipu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atamwangalia yule mutu. Kuhani akiona pamekuwa shimo na nywele za pahali pale zimegeuka kuwa nyeupe, basi, kuhani atamutangaza mutu yule kuwa muchafu. Huo ni ugonjwa wa ukoma ambao umetokana na jipu.